Deuteronomy 4:16-19

16 aili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke, 17 bau kama mnyama aliye juu ya nchi au ndege yeyote arukaye angani, 18au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki yeyote aliye ndani ya maji. 19 cNa utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyo Bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu.
Copyright information for SwhKC